Katika siku ya nne ya programu ya mafunzo ya Internet kwa waandishi wa habari, tulifunzwa jinsi ya kuunganisha blogi yako na za watu wengine.
Mataalamu wetu Peik Johansson alitufundisha njia ambazo unaweza kuunganisha blogi yako na watu wengine sambamba na yako kuunganishwa na watu wengine.
Aidha mtaalamu huyo aliendelea kutoa kazi za jinsi ya kutafuta habari mbali kwenye Internet lakini katika siku hiyo darasa lilijikita zaidi kwenye ufafutaji wa habari za michezo.
Mbali ya kusaka habari za michezo pia, wanafunzi tulipata fursa ya kuandikia maelezo na Profesa wa Kizanzibari Abdulrazak Gurnah, Fredie Mercury ambao ni Wazanzibari mashuhuri na waliojipatia umaarufu mkubwa sana nje ya visiwa hivi.
lakini pengine ukiwauliza Wazanzibari na pengine Watanzania waliowengi wanaweza wasiwaelewe watu hawa waliojizolea sifa na tunzo kadhaa za uandishi wa vitabu na muziki.
Aidha pia katika kusaka habari hizo tuliangalia tamasha la Sauti za Busara ambalo limefunguliwa rasmi hapa Zanzibar.
Katika mafunzo yake alisisitiza haitakiwi kwa mtu yeyote kunukuu kama ilivyo kutoka kwenye mtandao, blogi ama chapisho lolote la mtu mwengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment